TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NA MAJIMBO MAPYA
Haya tena kwa wale wenye interest na haya masuala
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UGAWAJI WA MAJIMBO NA RATIBA YA UCHAGUZI MKUU WA 2010”
1.Ugawaji wa Majimbo
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,Kwa mamlaka iliyopewa chini ya Ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,inawatangazia wadau wa Uchaguzi na Wananchi kwa ujumla kuwa itagawa Majimbo ya Uchaguzi yafuatayo.
i.Nkasi
ii.Tunduru
iii.Maswa
iv.Kasulu Mashariki
v.Bukombe
vi.Singida Kusini
vii.Ukonga
Taarifa zaidi kuhusu Majimbo hayo mapya yatakayoanzishwa itatolewa baada ya Tume kukutana na wadau wa Majimbo husika.
2. Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa 2010
Kwa mujibu wa Vifungu vya 37(1)(a) na 46(1) vya Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Vifungu vya 41(1) na 48(1) vya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ,Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi pia inawatangazia Wananchi wote kuwa Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 kwa Uchaguzi wa Rais, Bunge na Madiwani itakuwa kama ifuatavyo;
1. UTEUZI WA WAGOMBEA - 19 AGOSTI,2010
2. KAMPENI ZA UCHAGUZI -20 AGOSTI, HADI 30 OKTOBA,2010
3. UPIGAJI KURA 31 OKTOBA, 2010
Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Tume itawatangazia Wananchi rasmi, tarehe ya kutoa Fomu za Uteuzi kwa wagombea.
JAJI MSTAAFU LEWIS M.MAKAME
MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Source: Jamiiforums
0 Comments:
Post a Comment
<< Home