Kijijini kifungua kinya saaafi kabisa. This time nilijikumbusha "mabumunda!". Wakati tukisoma mjin i Mbeya ukila kipande ukashushia glasi ya maji......siku imepita!
Daraja hili lilijengwa kuelekea kwenye vibanda hivyo vinavyoonekana katika picha. Haliendi kwingine kokote! Baada ya vibanda hiyvyo ni milima tu! Ama kweli daraja hili kitendawili
Niliwahi kutumia takriban miaka kumi ya uhai wangu katika nyumba hii. Ndiyo nyumba ya kwanza kuishi katika utumishi wangu serikalini bara baada ya kumaliza shule
Zamani kielelezo cha Stone City kilikuwa ile miamba maarufu ya Bismaki iliyo ziwani pale kwenye Ferry ya kuendea Kamanga. Kwa sasa kuna hii sanamu ya Sangara inapanda chati
Nimeanza kuyafaidi maembe haya baada ya kuyapand miaka mitatu iliyopita. Miche niliinunua pale TTSA MOROGORO. Nadhani yanaitwa "Matombo Sweet" na kweli ni matamu