Mwambegele

Thursday, March 31, 2011

VICTORIA, MAHE SEYCHELLES




Mitaa ya Ushelisheli

VICTORIA, MAHE SEYCHELLES




Niliambiwa kuwa mnara wa saa ni kielelezo cha Jiji la Victoria, Mahe Seychelles

KISIWA CHA PARADISO





Kisiwa cha paradiso kinavyoonekana kutoka kilimani

KISIWA CHA PARADISO





Paradise Island, Seychelles. Hiki ni kisiwa cha kutengenezwa na binadamu. Udongo ukajazwa mpaka kikapatikana. Bado ujenzi wake haujakamilika. Baada ya kukamilika kila mwenye nyumba huko atakuwa na mahali pa kuegesha boti lake baharini kama inavyoonekana. Hata hivyo, niliambiwa kuwa huko kutakuwa mahali ghali sana siyo kwa kila Juma, Joni na Haji yeyote kuishi huko

MAIA LUXURY RESORT





Hapa ni Maia Luxury Resort. Mwenyeji wangu aliniambia kuwa hii Resort maarufu kwa watu maarufu hasa Celebrities. Aliniambia kuwa kwa usiku mmoja hazipungui paundi za Kiingereza elfu moja. Kwa hela ya Ki-TZ nika milioni mbili na ushei hivi.

APPLE CHUNGU



Sijawahi kuliona tunda la aina hii. Nililiona Victoria Mahe, Seychelles. Niliambiwa linaitwa bitter apple

MAPERA



Pera ni tunda lenye vitamin C kushinda matunda mengi sana

PARACHICHI




Kijijini kwetu kuna maparachichi. Lakini kwa kweli tangu nizaliwe sijawahi kuona mparachichi (kienyeji tunaita mkatapera) uliozaa maparachichi (tunayaita makatapera) mengi kama huu. Mparachichi huu niliuona kisiwa cha Mahe, Seychelles..