Mwambegele

Monday, June 28, 2010

MENU


Hii ni "menu" ya ugali, mtindi na parachichi. Rafiki yangu Nico amesema alikuwa anaifurahia sana "menu" hii miaka ya 1970 alipokuwa akiipata pale Nzovwe, Jijini Mbeya.

MABATINI, MWANZA


Mabatini, Mwanza

JIJI LA MWANZA





Jiji la Mwanza linavyoonekana kutoka kilima cha Kitangiri, Kirumba.

TOWER OF LONDON


Kibao hiki kipo Tower of London. Kwa kweli kwa wanahistoria kibao hiki kinaonyesha jinsi jamii ilikotoka mbali.

MLIMA RUNGWE


Mlima Rungwe huonekana karibu kila sehemu ya Wilaya ya Rungwe. Hapa mlima Rungwe unavyoonekana kutoka kiijijini Lugombo. Kijiji hiki kiko kwenye njia inayo kwenda Chuo cha Magereza.

TUKUYU



Mji wa Tukuyu kama unavyoonekana kutoka kijijini Bujinga. Karibu kidogo na picha ni kanisa Kuu la Moravian na Shule ya Msingi Bagamoyo. Nilisoma hapo enzi hizo ikiitwa Aga Khan Primary School.

UFUGAJI TUKUYU




Ng'omge hawa (kutoka zizi hili) nilikuwa nikishiriki kuwachunga machungani. Siku hizi wafungaji wengi wanatumia ufugaji wa zero grazing kwa sababu ya kukosa sehemu za malisho. Hapa mfugaji wa kijiji cha Bujinga, Tukuyu , akilisha mifugo yake kwa mtindo wa zero grazing.

Friday, June 25, 2010

KUAPISHWA KWA JAJI SONGORO



Akiwa na familia

KUAPISHWA KWA JAJI SONGORO


Alipata nafasi ya kusalimiana na Rais Mstaafu William (Bill) Jefferson Clinton

HARUNA TWAIB SONGORO



Tarehe 22 Juni, 2010 Rais Jakaya Mrisho Kikwete alimwapisha HARUNA TWAIB SONGORO kuwa jaji wa Mahakama Kuu. Jaji Songoro alinipokea mimi kazini na kunifundisha kazi ya Wakili wa Serikali miaka ishirini iliyopita.

KUAPISHWA KWA JAJI SONGORO


Na majaji wenzake

KUAPISHWA KWA JAJI SONGORO

akiwa na familia

KUAPISHWA KWA JAJI SONGORO

Alipata nafafasi ya kusalimiana na Rais mstaafu William (Bill) Jefferson Clinton

HARUNA TWAIB SONGORO

Tarehe 22 Juni, 2010 Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliwaapisha majaji kumi; mmojawapo alikuwa ni rafiki yangu wa muda mrefu: Haruna Twaib Songoro. Huyu Wakili ndiye aliyenipokea na kunifundisha kazi wa Wakili wa Serikali. Nakutakia kila la kheri kwenye kazi yako mpya.

Tuesday, June 22, 2010

UKILI WA KYUSA


Mama yangu hupenda sana kusuka ukili.
Nimekuwa nikimuona hivi tangu aliponizaa.